Description

Hongera sana na karibu katika safari ya kuvunja vifungo vya nafsi na kurejesha uhuru wako katika Kristo YESU.

Vifungo vya nafsi, ingawa mara nyingi havionekani, vina nguvu kubwa na madhara makubwa katika maisha ya wengi. Katika mwongozo huu, tunaangalia maana ya vifungo vya nafsi, vyanzo vyake, madhara yake na namna ya kutoka kwenye vifungo hivyo. Kwenye mwongozo huu pia kuna namna ya kuomba kwa siku saba hatua kwa hatua ili uweze kuwekwa huru kabisa.

Kila jambo linalotokea katika maisha ya mwanadamu lina chanzo katika ulimwengu wa roho. Katika mwongozo huu, Mungu ametupa neema ya kutufundisha kuhusu vifungo vya nafsi na jinsi ya kutoka katika nira za kishetani. Biblia imeandika kwamba watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa (Hosea 4:6), ndiyo maana Mungu ametupa fursa ya mwongozo huu ili kila mtu aweze kupata maarifa ya kujinasua kutoka kwenye vifungo na kuishi maisha ya furaha na ushindi. Maana mawazo anayotuwazia Mungu ni mema (Yeremia 29:11-14). Tunakuombea kwa jina la Yesu kwamba ufahamu wako ufunguke na upokee msaada kupitia maarifa haya.

Utakaposoma mwongozo huu pamoja na maombi yake, Roho Mtakatifu ambaye ndiye kiongozi wa huduma hii atakuwa nawe katika kila hatua, na madhihirisho yake yataonekana waziwazi. Huu siyo tu mwongozo wa kusoma, bali ni mwongozo wenye matendo na matokeo ya moja kwa moja, hivyo soma na tekeleza kila kitu kwenye maelekezo haya. Ubarikiwe sana.

Reviews

There are no reviews yet.

Only logged in customers who have purchased this product may leave a review.