Description
Kwa kipindi cha muda mrefu sasa ibilisi amewekeza kwa kiasi kikubwa kuharibu taasisi ambayo kwa sasa inapitia mambo mengi yanayopelekea jina la Mungu halitukuzwi katika ngazi hiyo. Baadhi ya mambo hayo ni kama kutengana kwa familia, migogoro ya mara kwa mara, magonjwa, uadui ndani ya familia, majanga mbalimbali nk. Kama maandiko yasemavyo Yohana 10:10 “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”
Katika kutekeleza hili, ibilisi amekua akinyanyua vita mbali mbali ikiwemo kunyanyua roho za giza rasmi na kuziweka juu ya familia ili kuzitawala kwa lengo la kutesa familia na kuhakikisha kabisa Mungu anashindwa kuabudiwa katika ngazi hii. Kuanguka kwa familia ndio kuanguka kwa kanisa, na nchi kwa ujumla. Ufunuo 13: 7- 8 “Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.”
Reviews
There are no reviews yet.